Dawa za kulevya: Mkoani Rukwa wakituhumiwa kulima, kuuza na kusafirisha dawa za kulevya ikiwemo heroin kufuatia msako maalumu kwa lengo la kukabiliana na uhalifu huo.



Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi mkoani Rukwa, msako huo ambao umefanyika hivi karibuni katika wilaya zote na kusimamiwa na kamati za ulinzi na usalama, mashamba ya bangi yenye ukubwa wa ekari 19 yameteketezwa kwa moto na bangi yenye uzito wa kilo 15 na misokoto 105 ya bangi imekamatwa ambapo heroin iliyokuwa ikisafirishwa kutoka jijini Mbeya kwenye mjini Sumbawanga imekamatwa.
Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi mkoani Rukwa, Mtatiro Nyamhanga ametangaza rasmi vita dhidi ya dawa za kulevya mkoani humo huku wakazi wa kijiji cha Msila ambacho ni maarufu kwa kilimo cha bangi wakiungana na Mwenyekiti wao kulishukuru Jeshi la Polisi kwa msako huo huku wakiwasihi wanaojihusisha na kilimo hicho haramu kuacha mara moja.

Amesema mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanafanyika katika wilaya zote Nkasi, Kalambo na Sumbawanga zenye jumla ya halmashauri nne mkoani Rukwa.
Wilayani Kalambo, Mkuu wa Wilaya hiyo, Julieth Binyura amethibitishwa kukamatwa kwa watu watano wakituhumiwa kulima bangi kwenye mashamba ya ukubwa wa ekari saba katika kijiji cha Ngoma, Kata ya Katete inayopakana na nchi jirani ya Zambia.
Binyura amewaagiza maofisa watendaji wa vijiji na kata zilizopo wilayani humo kuwabaini wanaolima bangi na kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili hatua za haraka zichukuliwe huku akionya kuwa wakishindwa kufanya hivyo, kila mtumishi wa umma aliyeko katika maeneo hayo ya utawala wasaidie kuwafichua wahalifu hao.
Wilayani Nkasi watu wawili wakazi wa kijiji cha Nkundi kilichopo katika Kata ya Kipande wilayani humo wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kulima bangi.
Waliokamatwa wametajwa kuwa ni pamoja na Oscar Msangawale na Thobias Malambo waliokutwa wanalima bangi kwenye mashamba yao na bustani zao kwa pamoja yakiwa na ukubwa wa ekari moja.
Katibu Tawala wa Wilaya Nkasi , Festo Chonya alidai kuwa walipata taarifa za kuwapo kwa shamba la bangi katika kijiji hicho ambapo Kamati ya Ulinzi na Usalama ilifika eneo la tukio na kukuta bangi ikiwa imelimwa katika shamba lenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja.
Akifafanua, alisema shamba la bangi lenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja linamilikiwa na Msangawale ambapo Malambo yeye alikutwa na bangi ikiwa imeoteshwa kwenye bustani ya maua iliyopo pembeni ya nyumba yake ya kuishi. Kufuatia msako huo, Polisi walifanikiwa kuiteketeza kwa moto bangi yote iliyovunwa katika shamba hilo.

Popular posts from this blog

Blowser error: Invalid Server Certificate

TANZANIA: MPANGO WA KUTENGENEZA ROBOT