MBUNGE wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, aomba maji ya mwekezaji



Amewaombea wananchi wa kijiji cha Pingo maji kwa mwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza vigae cha Twyford, anayetarajia kuyavuta kutoka mto Ruvu hadi kiwandani kwake.
Ridhiwani ameomba ombi hilo mwishoni mwa wiki wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho uliofanywa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.
Amesema wananchi hao wamekuwa na shida ya maji kwa kipindi kirefu tangu nchi ipate uhuru, hivyo wakati muwekezaji huyo atakapovuta maji katika kiwanda chake awasaidie na wananchi hao kupata huduma hiyo.
"Mheshimiwa Waziri tuna tatizo la maji, wananchi wa kijiji hiki wamesubiri maji tokea uhuru, tunaomba utuombee kwa mwekezaji wakati akiyavuta kutoka mto Ruvu, wananchi nao wafaidike," alisema Mbunge huyo huku akipongezwa na wananchi wake.
Hata hivyo, wakati wa akitoa hotuba yake, Mwijage alimuomba mwekezaji huyo kusaidia kuwapamaji wananchi hao, jambo alilolikubali kulitekeleza kwa gharama zake.
Mwijage alifafanua kuwa kiwanda hicho kitahitaji maji lita 900,000 katika shughuli zake za uzalishaji, ambapo awali maji hayo yalipangiwa kutoka mto Wami.
"Ruvu inapitisha lita milioni 201, ukawaomba walete lita milioni moja huku kwa ajili ya mahitaji ya kiwanda, Mkurugenzi wa Dawasa alikubali," alisema.
Mwijage pia alimuomba mwekezaji huyo asaidie kupeleka maji mpaka Chalinze mjini ambapo alikubali pia.
"Mnaona matunda ya viwanda, si tu kwenye kukuza uchumi bali pia kuboresha huduma zakijamii kama hizi. Tunawashukuru sana na niwaombe tu wananchi ili kufanikisha upatikanaji huo wa maji msidai fidia pale ambapo bomba hilo litapita,” alisistiza.

Popular posts from this blog

Blowser error: Invalid Server Certificate

TANZANIA: MPANGO WA KUTENGENEZA ROBOT