MTANZANIA
OPERESHENI: Upambanaji zidi ya madawa ya kulevya, DC Makonda
“Hata kama ni askari wetu watabainika kujishughulisha na uhalifu, hatuwezi kumvumilia hata kidogo kwenye hili,” alisema IGP Mangu.
“Kundi hili la watu ndio nguvu kazi ya taifa letu. Kwa hiyo tunaona ni kwa namna gani tunapoteza nguvu kazi ya taifa, hivyo ni vema wakati tunaadhimisha Siku ya Saratani Duniani tukaepuka viashiria vya ugonjwa huu, ikiwa ni pamoja na matumizi ya pombe,” alisema Profesa Magimba.
Reli hiyo ambayo awamu yake ya kwanza itakuwa na urefu wa kilometa 300, itaiwezesha Tanzania kutumia treni ya umeme yenye kusafiri kwa kasi ya kilomita 160 kwa saa.
Kukamilika kwa reli hiyo kutaifanya Tanzania kwenda sanjari na India ambayo nayo tayari ina treni yenye kusafiri kwa kasi ya kilometa 160 kwa saa kutoka New Delhi hadi Agra.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kutembelea Hoteli ya Aishi, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Byakanwa, alisema amepata taarifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa jalmashauri hiyo kuwa Mbowe amekwepa kulipa kodi ya huduma ya biashara kwa takribani miaka mitano iliyopita.
“Hatufanyi hivi kwa kumwonea mtu, bali ni kwa mujibu wa sheria na endapo mtu atafuata sheria hakuna wa kumfuata, kila mtu ni lazima afuate utaratibu bila kujali cheo alichonacho,” alisema.
MPINZANI WA NAPE 2015 AFUNGWA JELA
Mathew ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa
wa Lindi na kiongozi mwenzake wa kata wamehukumiwa kwenda jela baada ya
kupatikana na hatia ya kufanya mkusanyiko bila ya kibali. Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya
Mkoa wa Lindi, mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mhina.
“Tutakata rufaa kupinga uamuzi huu, leo naandaa
barua ya kuomba nakala ya hukumu ili tuanze kuandaa rufaa ya wateja wangu,”
alisema Wakili Kamalamo. Read more













