MBUNGE wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, aomba maji ya mwekezaji
Amewaombea wananchi wa kijiji cha Pingo maji kwa mwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza vigae cha Twyford, anayetarajia kuyavuta kutoka mto Ruvu hadi kiwandani kwake. Ridhiwani ameomba ombi hilo mwishoni mwa wiki wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda hicho uliofanywa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage. Amesema wananchi hao wamekuwa na shida ya maji kwa kipindi kirefu tangu nchi ipate uhuru, hivyo wakati muwekezaji huyo atakapovuta maji katika kiwanda chake awasaidie na wananchi hao kupata huduma hiyo. "Mheshimiwa Waziri tuna tatizo la maji, wananchi wa kijiji hiki wamesubiri maji tokea uhuru, tunaomba utuombee kwa mwekezaji wakati akiyavuta kutoka mto Ruvu, wananchi nao wafaidike," alisema Mbunge huyo huku akipongezwa na wananchi wake. Hata hivyo, wakati wa akitoa hotuba yake, Mwijage alimuomba mwekezaji huyo kusaidia kuwapamaji wananchi hao, jambo alilolikubali kulitekeleza kwa gharama zake. Mwijage alifafanua kuwa kiwand...